# TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI

- Link: https://kilimanjaroyetu.com/2026/10/28/tangazo-la-nafasi-za-kazi-halmashauri-ya-wilaya-ya-hai/
- Published: 2026-10-28T13:44:52+00:00
- Author: 

**tangazo la nafasi za kazi halmashauri ya wilaya ya hai** is an official job vacancies
published by Ajira Tanzania on 28 October 2026.

## Announcement Details

**Announcement type:** Job Vacancies

**Official reference:** 9f521554-f164-452b-b49b-dbf05dc0236c

**Deadline:** 10 November 2026

## Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Hai

## Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

## Ofisi Ya Rais

## Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa

## Halmashauri Ya Wilaya Ya Hai

(Barua zote zitumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji)

Kumb.Na.LG/B.20/2/195 Tarehe: 28/10/2026

## Tangazo La Nafasi Za Kazi

## (Linarudiwa)

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai anawatangazia Watanzania

wenye sifa kuomba nafasi za kazi kumi na mbili (12) katika Halmashauri hii baada
ya

kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

kwa mchanganuo ufuatao:-

## 1.0 Dereva Daraja La Ii – Nafasi 07

## 1.1 Majukumu Na Kazi

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;

ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbali mbali kwenye safari za kikazi;

iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;

iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;

v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;

vi. Kufanya usafi wa gari;

vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

## 1.2 Sifa Za Mwombaji

Kuajiriwa wenye elimu ya kidato cha Nne (Form IV) na leseni ya Daraja E au C ya 
uendeshaji

magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha

ajali,pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
Vilevile wawe

wamehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa

na vyuo vyovyote vinavyotambuliwa na serikali.

## 1.3 Ngazi Ya Mshahara

## Tgs B

## 2.0 Mwandishi Mwendesha Ofisi Ii – Nafasi 05

## 2.1 Kazi Na Majukumu

i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za Siri;

ii. Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaeleza

wanapoweza kusaidiwa;

iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao,

safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;

iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa

majukumu ya kazi;

v. Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara /

Kitengo/ Sehemu husika, Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada

na nyaraka sehemu zinazohusika;

vi. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;

vii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi;

viii. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

## 2.2 Sifa Za Mwombaji

Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne au Sita mwenye Stashahada (Diploma)

ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha, awe amefaulu somo la

Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno100 kwa dakika moja na kupata

program za Kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, internet, email
na

Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

## 2.3 Ngazi Ya Mshahara

## Tgs C

## Masharti Ya Jumla

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi

miaka 45;

ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na

wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao

kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;

iii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na

Mwanasheria/Wakili;

iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed

C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya

wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;

v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za

vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya

Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na

vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi

husika. Postgraduate/ Degree/ Advanced Diploma/ Diploma/

Certificates, -Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer

Certificate, -Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from

respective boards);

vi. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo

za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)

## Havitakubaliwa;

vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao

vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na

## Nacte);

viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi

kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia

walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia

maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe

30 Novemba, 2010;

x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa

hatua za kisheria;

xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 10 Novemba, 2026;

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa

pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

## Mkurugenzi Mtendaji (W),

## Halmashauri Ya Wilaya Ya Hai,

## S. L. P 27,

## Hai.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira Recruitment Portal

kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana 
kwenye

tovuti ya Seckretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment

Portal’).Aidha, maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika

tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Limetolewa na;

## Mkurugenzi Mtendaji (W)

## Halmashauri Ya Wilaya Ya Hai

4

## Official Source

Verify names, dates, requirements and instructions in the official PDF published
by Ajira Tanzania.
