# TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NANYUMBU

- Link: https://kilimanjaroyetu.com/2026/11/07/tangazo-la-nafasi-za-kazi-halmashauri-ya-wilaya-ya-nanyumbu/
- Published: 2026-11-07T18:26:58+00:00
- Author: 

**tangazo la nafasi za kazi halmashauri ya wilaya ya nanyumbu** is an official job
vacancies published by Ajira Tanzania on 07 November 2026.

## Announcement Details

**Announcement type:** Job Vacancies

**Official reference:** 5d28c2c3-86d1-480e-9f4c-b15059be68ff

**Deadline:** 13 November 2026

## Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Nanyumbu

Kumb.Na.NDC/L10/1/VOL IX/3 Tarehe 06.11.2026

## Tangazo La Nafasi Za Kazi

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu anawatangazia watanzania

wenye sifa za kuomba nafasi za kazi saba (07) katika Halmashauri hii baada ya

kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala

Bora kwa mchanganuo ufuatao:-

## 1.0 Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La Ii – Nafasi 4

## 1.1.1 Majukumu Ya Kazi

i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri,

ii. Kupokea wageni na kuwasilisha shida zao na kuwaelekeza wanapoweza

kusaidiwa;

iii. Kutunza taarifa za Kumbukumbu ya matukio, miadi,tarehe za vikao, safari za 
Mkuu

wake na ratiba za kazi zingine.

iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya

kazi;

v. Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Divisheni, Vitengo

na Sehemu zinazohusika;

vi. Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;

vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali; na

viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

## 1.1.2 Sifa Za Mwombaji

Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) na

amehitimu Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha

wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa Dakika

moja na kupata programu za kompyuta za Ofisi kama vile; word, Excel, Powepoint,

Internet, E-mail na Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

## 1.1.3 Ngazi Ya Mshahara

## Tgs C

## 2.0 Dereva Daraja La Ii – Nafasi 3

## 2.1.1 Majukumu Ya Kazi

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.

ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.

iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.

iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.

v. kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.

vi. kufanya usafi wa gari, na

vii. kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

## 2.1.2 Sifa Za Waombaji

Kuajiriwa mwenye Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au

C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka

mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa

ya kupata madaraja husika. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji

magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha VETA au Chuo kingine

kinachotambuliwa na Serikali.

## 2.1.3 Ngazi Ya Mshahara

## Tgs B

## Masharti Ya Jumla

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45,

ii. Waombaji waambatanishe Cheti cha Kuzaliwa,

iii. Waombaji waambatanishe melezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V)

yenye Anwani, Namba za Simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini

(Referees) wa kuaminika,

iv. Waombaji wote waweke nakala za vyeti vya taaluma na vyeti vya Kidato cha

Nne na Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo

mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika kwenye Ajira Portal,

v. Testimonials “Provision Results”, “Statement of Results” Hati ya Matokeo

ya Kidato cha Nne na Sita HAVIKUBALIKI,

vi. Waombaji wa kazi ya Kada ya Dereva II wenye Leseni Daraja E au C

wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa

ya kupata madaraja husika.

vii. Waombaji wote waweke picha mbili “Passport Size” ya hivi karibuni katika

ukurasa wa Ajira Portal,

viii. Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na

kuthibitishwa na mamlaka husika yaani TCU, NECTA na NACTE,

ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba

isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi,

x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika

Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo

katika Waraka wenye Kumb. Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba,

2010,

xi. Uwasilishwaji taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za

kisheria,

xii. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 19 November, 2026,

xiii. MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa

pamoja na vyeti vya Elimu, Anwani ya barua hiyo ielekeze kwa:-

Mkurugenzi Mtendaji (W),

Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu,

## S.L.P. 246,

## Nanyumbu- Mtwara.

xiv. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira

(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani

hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu

iliyoandikwa 'Recruitment Portal').

xv. Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili

## Hayatafikiriwa.

Tangazo hili limetolewa na:

Ibrahim J. Mwanauta

## Mkurugenzi Mtendaji

## Halmashauri Ya Wilaya Nanyumbu

## Official Source

Verify names, dates, requirements and instructions in the official PDF published
by Ajira Tanzania.
