# TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA KUJITOLEA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA

- Link: https://kilimanjaroyetu.com/2026/11/13/tangazo-la-nafasi-za-kazi-za-kujitolea-halmashauri-ya-wilaya-ya-bukoba/
- Published: 2026-11-13T14:57:03+00:00
- Author: 

**tangazo la nafasi za kazi za kujitolea halmashauri ya wilaya ya bukoba** is an
official job vacancies published by Ajira Tanzania on 13 November 2026.

## Announcement Details

**Announcement type:** Job Vacancies

**Official reference:** 06850279-4e1d-4551-9322-23c76092873d

**Deadline:** 19 November 2026

## Tangazo La Nafasi Za Kazi Za Kujitolea Halmashauri Ya Wilaya Ya Bukoba

## Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

## Ofisi Ya Waziri Mkuu

## Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa

## Halmashauri Ya Wilaya Ya Bukoba

(Barua zote ziandikwe kwa Mkurugenzi Mtendaji)

Kumb. Na. HB.21/401/01/15

13 Novemba, 2026

## Tangazo La Nafasi Za Kazi Za Kujitolea

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwa kuzingatia mwongozo

wa kujitolea katika Utumishi wa Umma wa Mwaka 2025 anawatangazia Watanzania

wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba

kuomba nafasi ya kazi tajwa hapo chini.

## 1.0 Dereva Daraja La Ii (Nafasi 03)

## 1.1. Sifa Za Mwombaji

Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya

uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1)

bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata

madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari

(Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine

kinachotambuliwa na Serikali.

## 1.2. Majukumu Ya Kazi

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;

ii. Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi;

iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;

iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;

v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari; na

vi. Kufanya usafi wa gari.

## Masharti Ya Ujumla

i. Mwombaji wa kujitolea awe raia wa Tanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18

na usiozidi miaka 35 na awe hajawahi kuajiriwa katika Taasisi yoyote ya Umma

ii. Mwombaji aambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye

anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini

(referees) watatu wa kuaminika.

iii. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, vilivyothibitishwa na

Mwanasheria/Wakili wa Serikali ambavyo ni kitambulisho cha Taifa/Namba ya

kitambulisho, Picha mbili za Passport za rangi, cheti cha kuzaliwa, cheti cha

Kidato cha Nne, cheti cha Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na

vyeti vya kuhitimu mafunzo mbali mbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.

iv. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo
za

Kidato cha Nne na Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)

## Havitakubaliwa.

v. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na

kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).

vi. Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za

kisheria.

vii. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25 Novemba, 2026.

viii. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa

pamoja na vyeti vya elimu, maombi yote yaelekezwe kwa;-

## Mkurugenzi Mtendaji (W),

## Halmashauri Ya Wilaya Ya Bukoba,

## S.L.P 491,

## Bukoba.

Limetolewa na:

## Mkurugenzi Mtendaji

## Halmashauri Ya Wilaya Ya Bukoba

## Official Source

Verify names, dates, requirements and instructions in the official PDF published
by Ajira Tanzania.
