TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU
tangazo la nafasi za kazi halmashauri ya wilaya ya magu is an official job vacancies published by Ajira Tanzania on 13 November 2026.
Announcement Details
Announcement type: Job Vacancies
Official reference: 825cceaf-9357-4fc4-b2ab-e737bcd947bc
Deadline: 26 November 2026
Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Magu
Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Ofisi Ya Rais.
Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa
Halmashauri Ya Wilaya Ya Magu
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb.Na. FA97/22B/01/A/25 13 Novemba, 2026
Tangazo La Nafasi Za Kazi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) ya Magu anawatangazia Watanzania wenye
sifa kuomba nafasi za kazi tatu (03) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali
kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kama
ifuatavyo:-
1.0 Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La Ii (Office Management
Secretary Grade Ii)- Nafasi 3
1.1.1 Majukumu Na Kazi
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
ii. Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza
kushughulikiwa.
iii. Kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari
za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya
kazi
v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika
vi. Idara/Kitengo/Sehemu husika
vii. Kukusanya, kutunza na kurejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
viii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi maandalizi ya vikao mbalimbali
ix. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi
1.1.2 Sifa Za Muombaji.
Kuajiriwa Wahitimu wa kidato cha Nne (IV) wenye Stashahada (Diploma) ya
Uhazili au cheti cha N TA level 6 ya Uhazili. Aidha, wawe wamefaulu somo la
Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata
program za komputa kama vile• Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail and
Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya
Halmashauri ya Wilaya ya Magu, 1078 Barabara ya Musoma, 334021078 Ilungu, Magu Mwanza
1.1.3 Ngazi Ya Mshahara
Tgs C
Masharti Ya Jumla Kwa Waombaji
i. Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na
usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
iii. Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa
KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata
madaraja husika.
iv. Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail
Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na
Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini
(Referees) watatu wa kuaminika.
v. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale
waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika Diploma/ Certificates, – Cheti cha mtihani wa
Kidato cha IV na VI,- Computer Certificate,-Vyeti vya Kitaaluma
(Professional Certificate from Respective Boards).
vii. “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya
Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
Havitakubaliwa.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi;
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya
Halmashauri ya Wilaya ya Magu, 1078 Barabara ya Musoma, 334021078 Ilungu, Magu Mwanza
xi. Mwisho wakutuma maombi ya kazi ni tarehe 26 Novemba, 2026.
xii. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji (W),
S.L.P. 200,
Magu.
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa Kielekroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment
Portal”.
Tangazo hili limetolewa na;
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Magu
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya
Halmashauri ya Wilaya ya Magu, 1078 Barabara ya Musoma, 334021078 Ilungu, Magu Mwanza
Official Source
Verify names, dates, requirements and instructions in the official PDF published by Ajira Tanzania.
Opportunity status: Open
Application deadline: 26 November 2026, 23:59 EAT
About the author
Related posts
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA
