Skip to content
Job Vacancies November 6, 2026

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOMBA

November 6, 20264 min read
tangazo la nafasi za kazi halmashauri ya wilaya ya momba

tangazo la nafasi za kazi halmashauri ya wilaya ya momba is an official job vacancies published by Ajira Tanzania on 06 November 2026.

Announcement Details

Announcement type: Job Vacancies

Official reference: df032fd7-8404-48e5-9f01-45ae3e07edc3

Deadline: 12 November 2026

Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Momba

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Ofisi Ya Waziri Mkuu

Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa

Halmashauri Ya Wilaya Ya Momba

Unapojibu tafadhali taja:

MODC/A10/38 VOL.III/29 06 Novemba, 2026

Tangazo La Nafasi Za Kazi Marudio

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba anawatangazia watanzania wenye sifa

kuomba nafasi za kazi mbili (2) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya

Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao:-

1.0 Dereva Daraja La Ii – Nafasi 02

1.1.1 Majukumu Na Kazi

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;

ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;

iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;

iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;

v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;

vi. Kufanya usafi wa gari; na

vii. Kufanya kazi zingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

1.1.2 Sifa Za Kuajiriwa

Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya

uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila

kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja

husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving

Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

1.1.3 Ngazi Ya Mshahara

Tgs B

1

1.1.4 Masharti Ya Jumla Kwa Waombaji

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na

usiozidi miaka 45.

ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa

kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;

iii. Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa

KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata

madaraja husika.

iv. Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum

Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua

Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa

kuaminika.

v. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika

Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika

Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.

vi. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na

Mwanasheria/Wakili.

vii. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na

Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia

kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi

husika Diploma/ Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI,-

Computer Certificate,-Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from

Respective Boards).

viii. “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato

cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)

Havitakubaliwa.

ix. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na

vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).

x. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba

isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi;

xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

2

xii. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 20 Novemba, 2026.

xiii. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja

na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-

Mkurugenzi Mtendaji,

Halmashauri ya Wilaya ya Momba,

S.L.P 273,

Momba.

xiv. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal)

kupitia anuani ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”

Limetolewa na;

Mkurugenzi Mtendaji (W)

Halmashauri Ya Wilaya Ya Momba

3

Official Source

Verify names, dates, requirements and instructions in the official PDF published by Ajira Tanzania.

Opportunity status: Open

Application deadline: 12 November 2026, 23:59 EAT

View Application Instructions

About the author