TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA KUJITOLEA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA
tangazo la nafasi za kazi za kujitolea halmashauri ya wilaya ya bukoba is an official job vacancies published by Ajira Tanzania on 13 November 2026.
Announcement Details
Announcement type: Job Vacancies
Official reference: 06850279-4e1d-4551-9322-23c76092873d
Deadline: 19 November 2026
Tangazo La Nafasi Za Kazi Za Kujitolea Halmashauri Ya Wilaya Ya Bukoba
Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Ofisi Ya Waziri Mkuu
Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa
Halmashauri Ya Wilaya Ya Bukoba
(Barua zote ziandikwe kwa Mkurugenzi Mtendaji)
Kumb. Na. HB.21/401/01/15
13 Novemba, 2026
Tangazo La Nafasi Za Kazi Za Kujitolea
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwa kuzingatia mwongozo
wa kujitolea katika Utumishi wa Umma wa Mwaka 2025 anawatangazia Watanzania
wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
kuomba nafasi ya kazi tajwa hapo chini.
1.0 Dereva Daraja La Ii (Nafasi 03)
1.1. Sifa Za Mwombaji
Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya
uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1)
bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata
madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari
(Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.
1.2. Majukumu Ya Kazi
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
ii. Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi;
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari; na
vi. Kufanya usafi wa gari.
Masharti Ya Ujumla
i. Mwombaji wa kujitolea awe raia wa Tanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18
na usiozidi miaka 35 na awe hajawahi kuajiriwa katika Taasisi yoyote ya Umma
ii. Mwombaji aambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
(referees) watatu wa kuaminika.
iii. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, vilivyothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili wa Serikali ambavyo ni kitambulisho cha Taifa/Namba ya
kitambulisho, Picha mbili za Passport za rangi, cheti cha kuzaliwa, cheti cha
Kidato cha Nne, cheti cha Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na
vyeti vya kuhitimu mafunzo mbali mbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
iv. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za
Kidato cha Nne na Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
Havitakubaliwa.
v. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
vi. Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za
kisheria.
vii. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25 Novemba, 2026.
viii. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, maombi yote yaelekezwe kwa;-
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri Ya Wilaya Ya Bukoba,
S.L.P 491,
Bukoba.
Limetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri Ya Wilaya Ya Bukoba
Official Source
Verify names, dates, requirements and instructions in the official PDF published by Ajira Tanzania.
Opportunity status: Open
Application deadline: 19 November 2026, 23:59 EAT
About the author
Related posts
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NANYUMBU
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOMBA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE
