Job Overview
Employer: MDAs & LGAs
Advert reference: Ajira #13541
Role: MUUGUZI II (NURSE II)
Open posts: 10 positions
Published: 13 June 2026
Deadline: 26 June 2026
Salary scale: TGHS A
Duties and Responsibilities
- Kufanya kazi za kiuguzi za kuhudumia wateja katika jamii, hospitali na sehemu zote zinapotolewa huduma za afya;
- Kusimamia na kuratibu kazi zote za wahudumu wa afya katika sehemu yake ya kazi;
- Kukusanya takwimu na kutayarisha taarifa za utendaji wake wa kazi;
- Kutoa huduma kwa wagonjwa majumbani;
- Kutoa ushauri nasaha;
- Kutoa huduma za kinga na uzazi wa mpango;
- Kutoa huduma za uzazi na afya ya mtoto;
- Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya;
- Kufuatilia utunzaji wa vitendea kazi katika maeneo yake ya kazi; na
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
Qualifications
Kuajiriwa wenye cheti cha uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania
How to Apply
Submit your application through the official Ajira Portal. Use the advert reference above if the portal opens at the vacancies list.
