JOBS August 2, 2026
NAHODHA DARAJA LA II (SKIPPER) at Halmashauri ya Wilaya ya Mafia
August 2, 20262 min read
Job Overview
Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Mafia
Advert reference: Ajira #13920
Role: NAHODHA DARAJA LA II (SKIPPER)
Open posts: 2 positions
Published: 31 July 2026
Deadline: 12 August 2026
Salary scale: TGS C
Duties and Responsibilities
- Kuendesha boti ya doria;
- Kubuni, kutengeneza na kutunza zana za kuvulia samaki (Fishing Gears);
- Kuongoza na kuendesha boti/meli ndogo zenye urefu wa futi 40 na uzito wa kuandikishwa wa tani 50 – 100 “Gross Tonnage (GRT)”;
- Kuendesha shughuli za uvuvi katika meli; Kushiriki katika kuendesha doria za baharini na nchi kavu, na Doria za EEZ;
- Kusoma taarifa za VMS na kuziwasilisha kwa Mkuu wa kituo kila siku, wiki, mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka;
- Kukamata wahalifu wa Sheria na Kanuni za Uvuvi;
- Kusaidia kutunza Kumbukumbu zote za matumizi ya mafuta katika vyombo vya doria;
- Kusaidia kuandaa ratiba ya kufanya matengenezo na “service” ya vyombo vyote vya doria (service schedule);
- Kutekeleza majukumu yote ya kikosi kama yalivyoainishwa katika Kifungu cha 32 cha Sheria ya Uvuvi na. 22 ya mwaka 2003; na
- Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wa kazi.
Qualifications
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI wenye Stashahada (Diploma NTA – level 6) ya Unahodha na Uvuvi (Master Fisherman) kutoka Vyuo vya Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (Fisheries Education and Training Agency – FETA) au sifa inayolingana na hiyo kutoka vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
How to Apply
Submit your application through the official Ajira Portal. Use the advert reference above if the portal opens at the vacancies list.