TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE
tangazo la nafasi za kazi halmashauri ya wilaya ya buhigwe is an official job vacancies published by Ajira Tanzania on 17 October 2026.
Announcement Details
Announcement type: Job Vacancies
Official reference: 0265b787-7e0d-4f9c-abc1-4282b3bdd707
Deadline: 23 October 2026
Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Buhigwe
Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Tawala Za Mikoa Na Serikali Za
Mitaa
REF:97/228/01A/25 15 Oktoba, 2026
Tangazo La Nafasi Za Kazi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe anakaribisha maombi ya kazi
kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 10 kama ilivyoainishwa
katika tangazo hili;
1.0 DEREVA DARAJA II (DRIVER II) – Nafasi 5
1.1 Majukumu Ya Kazi
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
ii. Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
iv. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
v. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali; na
vi. Kufanya usafi wa Gari;
1.2 Sifa Za Mwombaji
Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya
uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1)
bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata
madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari
(Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.
Page 1 of 4
1.3 Ngazi Ya Mshahara
Tgs B
2.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – Nafasi 5
2.1 Majukumu Ya Kazi
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri;
ii. Kupokea wageni na kuwasikiza shida zao na kuwaelekeza wanapoweza
kusaidiwa;
iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za
Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya
kazi;
v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu
husika;
vi. .Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mablimbali;
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; naix.Kufanya kazi zingine
atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
2.2 Sifa Za Mwombaji
Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six)
wenye Stashahada (NTA Level 6) ya Uhazili (Secretarial Studies). Aidha, wawe
wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 (80.w.p.m) kwa
dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word,
Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
2.3 Ngazi Ya Mshahara
Tgs.C
Masharti Ya Jumla
Page 2 of 4
1. Waombaji wote lazima wawe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi
umri wa miaka 45. Hata hivyo, kwa nafasi za ndani ya Taasisi za Kijeshi:
Waombaji wa nafasi zisizo za shahada wasizidi umri wa miaka 25.
Waombaji wa nafasi za shahada wasizidi umri wa miaka 30.
2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
3. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili.
4. Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba
CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
5. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti
vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
6. "Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato
cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
7. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET). Kwa waombaji wa
kada zinazohitaji 'GPA' waliosoma nje ya Tanzania waambatishe cheti cha ukokotozi
wa 'GPA' kutoka TCU.
8. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
9. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
10. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 30 Oktoba, 2026.
11. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti
vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji
Page 3 of 4
S.L.P 443, Kigoma
12. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal)
kupitia anuani ifuatayo;https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye
tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment
Portal').
13. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
Hayatafikiriwa.
14. Waombaji wote wa kazi wanakumbushwa kuwa ni marufuku kutoa au kupokea
rushwa kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi. Mchakato wa ajira
unazingatia misingi ya haki, usawa, na uwazi, kwa kuzingatia sifa stahiki
zilizoainishwa katika tangazo la kazi husika na muundo wa utumishi wa idara
inayohusika.
Limetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Page 4 of 4
Official Source
Verify names, dates, requirements and instructions in the official PDF published by Ajira Tanzania.
Opportunity status: Open
Application deadline: 23 October 2026, 23:59 EAT
About the author
Related posts
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBITI
