Skip to content
Job Vacancies October 20, 2026

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA

October 20, 20265 min read
tangazo la nafasi za kazi halmashauri ya wilaya ya iringa

tangazo la nafasi za kazi halmashauri ya wilaya ya iringa is an official job vacancies published by Ajira Tanzania on 08 October 2026.

Announcement Details

Announcement type: Job Vacancies

Official reference: a1339f2e-c5ac-4fb6-985c-118848bb2bbb

Deadline: 13 November 2026

Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Tawala Za Mikoa Na Serikali Za

Mitaa

KUMB.NA IDC/S/20/45/45 02 Oktoba, 2026

Tangazo La Nafasi Za Kazi

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa anawatangazia na kuwakaribisha

Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi 6 zilizoidhinishwa baada ya kupokea kibali

kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

kwa mchanganuo ufuatao;

1.0 Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La Ii – Nafasi 1

1.1 Majukumu Ya Kazi

i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri;

ii. Kupokea wageni na kuwasikiza shida zao na kuwaelekeza wanapoweza

kusaidiwa;

iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za

Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;

iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya

kazi;

v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu

husika;

vi. Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;

vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;

viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; na

ix. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

Page 1 of 4

1.1.2 Sifa Za Mwombaji

Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne au Sita na Stashahada (Diploma) ya Uhazili

au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya

Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za kompyuta

za ofisi kama vile:- Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo

chochote kinachotambuliwa na Serikali.

1.1.3 Ngazi Ya Mshahara

Tgs C

2.0 DEREVA DARAJA II (DRIVER II) – Nafasi 5

2.1. Majukumu Ya Kazi

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;

ii. Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;

iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;

iv. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;

v. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali; na

vi. Kufanya usafi wa Gari;

2.1.2 Sifa Za Mwombaji

Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya

uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1)

bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata

madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic

Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na

Serikali.

2.1.3 Ngazi Ya Mshahara

Tgs B

Page 2 of 4

Masharti Ya Jumla

1. Waombaji wote lazima wawe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi

umri wa miaka 45. Hata hivyo, kwa nafasi za ndani ya Taasisi za Kijeshi:

Waombaji wa nafasi zisizo za shahada wasizidi umri wa miaka 25.

Waombaji wa nafasi za shahada wasizidi umri wa miaka 30.

2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa

kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

3. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na

Mwanasheria/Wakili.

4. Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma,WASIOMBE na

wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba

CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

5. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti

vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya

kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-

Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

6. "Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato

cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

7. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na

kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET). Kwa waombaji wa

kada zinazohitaji 'GPA' waliosoma nje ya Tanzania waambatishe cheti cha ukokotozi

wa 'GPA' kutoka TCU.

8. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba

isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

9. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za

kisheria.

10. Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA

vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.

11. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 15 Oktoba, 2026.

12. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti

vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

Mkurugenzi Mtendaji

Page 3 of 4

S.L.P 108, Iringa

13. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal)

kupitia anuani ifuatayo;https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye

tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment Portal').

14. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili

Hayatafikiriwa.

15. Waombaji wote wa kazi wanakumbushwa kuwa ni marufuku kutoa au kupokea rushwa

kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi. Mchakato wa ajira unazingatia

misingi ya haki, usawa, na uwazi, kwa kuzingatia sifa stahiki

zilizoainishwa katika tangazo la kazi husika na muundo wa utumishi wa idara

inayohusika.

Limetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji

Page 4 of 4

Official Source

Verify names, dates, requirements and instructions in the official PDF published by Ajira Tanzania.

Opportunity status: Open

Application deadline: 13 November 2026, 23:59 EAT

View Application Instructions

About the author