Skip to content
Job Vacancies November 3, 2026

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE

November 3, 20264 min read
tangazo la nafasi za kazi halmashauri ya wilaya ya kisarawe

tangazo la nafasi za kazi halmashauri ya wilaya ya kisarawe is an official job vacancies published by Ajira Tanzania on 03 November 2026.

Announcement Details

Announcement type: Job Vacancies

Official reference: 04096795-7b6a-465f-919f-a50f43fa454d

Deadline: 09 November 2026

Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Kisarawe

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Ofisi Ya Waziri Mkuu

Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa

Halmashauri Ya Wilaya Ya Kisarawe

(Barua zote ziandikwe kwa Mkurugenzi Mtendaji (W)

Kumb.Na.KDC/SC.47/XV 03/11/2026

Tangazo La Nafasi Za Kazi

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe anakaribisha maombi

ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 04 kama

ilivyoainisha katika tangazo hili:-

1.0. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La Ii (Nafasi 04)

1.1. Kazi Na Majukumu

i. Kuchapa barua , taarifa na nyaraka za kawaida na za siri;

ii. Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu

wanapoweza kughughulikiwa;

iii. Kutunza taarifa / kumbukumbu za matukio, miada, wageni, tarehe za vikao,

safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine;

iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu

ya kazi;

v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/ Kitengo/

Sehemu husika;

vi. Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu

zinazohusika;

vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;

viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

1.1.2 Sifa Za Mwombaji.

Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (VI) na kupata cheti cha

Mtihani wa Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI). Awe na Stashahada (Diploma) ya

Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutoka katika Vyuo vinavyotambuliwa

na Serikali. Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno

100 kwa dakika moja. Awe amepata mafunzo ya programu za Komputa za ofisi

kama vile Word, Excel, Powe point, Internet, E-mail na Publisher.

1.1.3 Ngazi Ya Mshahara

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C

Masharti Ya Jumla Kwa Waombaji

i. Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia

miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa wale walioko kazini Serikalini;

ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na

wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu

walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa

Umma;

iii. Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail

Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu

zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na

majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.

iv. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko

katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia

maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe

30 Novemba, 2010.

v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu naTaaluma

vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, ambavyo ni vyeti vya Kidato

cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu

mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.

Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, –

Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI,- Computer Certificate,-

Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective

Boards).

vi. “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya

matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM

Vi Results Slips) Havitakubaliwa.

vii. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao

vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na

Nacte).

viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi

kuomba isipokuwa kama wanakibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi;

ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa

hatua za kisheria.

x. Mwisho wakutuma maombi ya kazini tarehe 20 Novemba, 2026.

xi. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi

iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe

kwa:-

Mkurugenzi Mtendaji,

Halmashauri Ya Wilaya Ya Kisarawe

S.L.P 28001,

Kisarawe

xii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira

(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;https://portal.ajira.go.tz/

(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa

kuingia sehemu iliyoandikwa ('Recruitment Portal').

xiii. Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika

tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Tangazo hili limetolewa na :

Mkurugenzi Mtendaji,

Halmashauri Ya Wilaya Ya Kisarawe

Official Source

Verify names, dates, requirements and instructions in the official PDF published by Ajira Tanzania.

Opportunity status: Open

Application deadline: 9 November 2026, 23:59 EAT

View Application Instructions

About the author