TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI
tangazo la nafasi za kazi halmashauri ya wilaya ya hai is an official job vacancies published by Ajira Tanzania on 28 October 2026.
Announcement Details
Announcement type: Job Vacancies
Official reference: 9f521554-f164-452b-b49b-dbf05dc0236c
Deadline: 10 November 2026
Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Hai
Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Ofisi Ya Rais
Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa
Halmashauri Ya Wilaya Ya Hai
(Barua zote zitumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji)
Kumb.Na.LG/B.20/2/195 Tarehe: 28/10/2026
Tangazo La Nafasi Za Kazi
(Linarudiwa)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai anawatangazia Watanzania
wenye sifa kuomba nafasi za kazi kumi na mbili (12) katika Halmashauri hii baada ya
kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
kwa mchanganuo ufuatao:-
1.0 Dereva Daraja La Ii – Nafasi 07
1.1 Majukumu Na Kazi
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbali mbali kwenye safari za kikazi;
iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
vi. Kufanya usafi wa gari;
vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.
1.2 Sifa Za Mwombaji
Kuajiriwa wenye elimu ya kidato cha Nne (Form IV) na leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji
magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha
ajali,pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Vilevile wawe
wamehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa
na vyuo vyovyote vinavyotambuliwa na serikali.
1.3 Ngazi Ya Mshahara
Tgs B
2.0 Mwandishi Mwendesha Ofisi Ii – Nafasi 05
2.1 Kazi Na Majukumu
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za Siri;
ii. Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaeleza
wanapoweza kusaidiwa;
iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao,
safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa
majukumu ya kazi;
v. Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara /
Kitengo/ Sehemu husika, Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada
na nyaraka sehemu zinazohusika;
vi. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
vii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi;
viii. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
2.2 Sifa Za Mwombaji
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne au Sita mwenye Stashahada (Diploma)
ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha, awe amefaulu somo la
Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno100 kwa dakika moja na kupata
program za Kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, internet, email na
Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
2.3 Ngazi Ya Mshahara
Tgs C
Masharti Ya Jumla
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi
miaka 45;
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na
wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao
kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
iii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili;
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed
C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya
wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za
vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya
Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na
vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
husika. Postgraduate/ Degree/ Advanced Diploma/ Diploma/
Certificates, -Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer
Certificate, -Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from
respective boards);
vi. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo
za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
Havitakubaliwa;
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na
Nacte);
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi
kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia
walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia
maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe
30 Novemba, 2010;
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa
hatua za kisheria;
xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 10 Novemba, 2026;
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri Ya Wilaya Ya Hai,
S. L. P 27,
Hai.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira Recruitment Portal
kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye
tovuti ya Seckretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment
Portal’).Aidha, maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika
tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Limetolewa na;
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri Ya Wilaya Ya Hai
4
Official Source
Verify names, dates, requirements and instructions in the official PDF published by Ajira Tanzania.
Opportunity status: Open
Application deadline: 10 November 2026, 23:59 EAT
About the author
Related posts
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA
